
Saa Heri ya Sala, No #137 Nyimbo za Kristo || Breath of Praise
1.1万回視聴・高評価数104
104________
‘Tis the Blessed Hour of Prayer
1. Saa heri ya sala tunapojidhili, Kama tukija kwake yesu rafiki. Tukiwa na imani kwamba yu mlinzi, Waliochoka sana watapata raha.
Saa ya sala, iliyo heri;
Waliochoka sana watapata raha.
2. Saa heri ya sala, ajapo mwokozi, Ili awasikie watoto wake. Hutwambia tuweke miguuni pake Mizigo yetu yote: tutapata raha.
3. Saa heri ya sala, wawezapo kuja Kwa Bwana Yesu wanaojaribiwa; Moyo wake mpole, atawarehemu; Waliochoka sana watapata raha.
4. Saa heri ya sala tutakapopewa Mibaraka ya roho, tukimwamini; Kwa kuamini kweli hatutaogopa; Waliochoka sana watapata raha
#breathofpraise #music #gospel
コメント